ICRC yasema hali ya ukame inatisha nchini Somalia
2022-03-17 07:55:30| CRI

ICRC yasema hali ya ukame inatisha nchini Somalia_fororder_VCG111368890162

Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) jana imeonya kuwa, hali ya ukame nchini Somalia inaendelea kuwa mbaya zaidi, na hatua za haraka zinatakiwa kuchukuliwa ili kukabiliana na hali hiyo.

Kiongozi wa ujumbe wa Kamati hiyo nchini Somalia Juerg Eglin amesema, Kamati yake imeanza kutekeleza operesheni ya kukabiliana na hali ya dharura ya ukame, ambayo inalenga maeneo yanayoathiriwa na migogoro na maeneo ambayo ni magumu kufikiwa.

ICRC inasema kuwa, watu zaidi 670,000 wamepoteza makazi yao kuanzia mwanzoni mwa Machi kutokana na kuongezeka kwa ukame.