Ghasia zinazoongezeka katika jimbo la Kivu Kaskazini nchini DRC zazuia usafirishaji wa misaada
2022-03-17 10:34:38| cri

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema kuwa ghasia kubwa zinazoongezeka kwenye sehemu ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zinaathiri vibaya usafirishaji wa misaada ya kibinadamu.

Ofisi hiyo ilisema kuwa tarehe 11 mwezi huu wapiganaji walifanya mashambulizi katika eneo la Beni huko Mambume na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 27, huku watu kadhaa wakiripotiwa kutoweka na nyumba kadhaa kuchomwa moto.

Ofisi hiyo ilisema kuongezeka kwa mashambulizi kulilazimisha mashirika saba ya misaada ya kibinadamu kusimamisha shughuli za utoaji wa misaada huko Kamango. Watu zaidi ya laki 3 hawakuweza kupata misaada ya kibinadamu katika maeneo ya Kamango, Mutwanga, Oicha na Mabalako kaskazini mwa Kivu Kaskazini.