Ethiopia yasifu uungaji mkono wa China katika maeneo mbalimbali
2022-03-18 08:37:20| CRI

Serikali ya Ethiopia imeisifu China kwa kuiunga mkono nchi hiyo katika maeneo mbalimbali ya ushirikiano.

Akizungumza na wanahabari jana mjini Addis Ababa, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia, Dina Mufti amesisitiza ushirikiano unaoendelea kukua kati ya nchi hiyo na China, na mabadilishano ya ngazi ya juu, kuaminiana kisiasa na kuboreka kwa uhusiano wa pande mbili.

Ameeleza umuhimu wa China kuiunga mkono Ethiopia katika majukwaa mbalimbali yaliyosaidia nchi hiyo kukabiliana na matishio ya mamlaka na ardhi yake.

Amesema kuongezeka kwa uhusiano kati ya pande hizo mbili kunadhihirika katika maeneo mbalimbali ikiwemo ujenzi, uendeshaji, na usimamizi wa reli ya SGR kati ya Addis Ababa na Djibouti, ambayo ni reli ya kwanza ya umeme inayovuka mpaka wa nchi.