Watu 19 wauawa katika shambulizi la kigaidi nchini Niger
2022-03-18 08:36:15| CRI

Watu 19 wauawa katika shambulizi la kigaidi nchini Niger_fororder_webwxgetmsgimg (2)

Watu 19 wameuawa wakiwemo polisi wawili katika shambulizi la kigaidi dhidi ya basi lililokuwa likitoka Burkina Faso kuelekea Tera magharibi mwa Niger Jumatano alasiri.

Washambuliaji waliokuwa wakiendesha pikipiki walilizuia basi hilo, na kuwafyatulia risasi abiria, na kuchoma moto basi hilo.

Katika miaka ya hivi karibuni, eneo linalojulikana kama “mipaka mitatu” (Niger-Mali-Burkina Faso) limeshuhudia mashambulizi yanayofanywa na makundi ya kigaidi dhidi ya vikosi vya usalama na raia.