Benki ya Dunia yaipatia Sudan Kusini dola milioni 120 za kimarekani kusaidia maendeleo ya miundombinu
2022-03-18 08:38:13| CRI

Sudan Kusini imesema imepokea dola za kimarekani milioni 120 kutoka Benki ya Dunia kupitia tawi lake la Shirikisho la Kimataifa la Maendeleo kwa ajili ya kuendeleza miundombinu nchini humo.

Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi nchini humo Agak Achuil Lual amesema, fedha hizo pia zitatumika kuimarisha taasisi za kijamii na kuboresha upatikanaji wa chakula nchini humo.

Naye mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Sudan Kusini Firas Raad amesema, mapigano yamewalazimisha mamilioni ya watu nchini Sudan Kusini kukimbia makazi yao, hivyo kuathiri utaratibu wao wa kijamii na kudhoofisa taasisi rasmi na zisizo rasmi nchini humo. Amesema fedha hiyo zitasaidia kuboresha miundombinu ya msingi, kuimarisha taasisi za kijamii, na pia kuboresha upatikanaji wa chakula.