Rwanda yafanya maonesho ya Wushu
2022-03-21 14:12:27| CRI

Shirikisho la Kungfu-Wushu la Rwanda Jumamosi lilifanya maonesho mbalimbali ya Kung Fu za kichina ili kukuza umoja kati ya wanachama wa shirikisho hilo.

Wachezaji wa Rwanda wakiwemo watu wazima na watoto waliwatumbuiza watazamaji kwa maonesho mbalimbali ya Kung Fu kama vile Tai Chi na Wing Chun kwenye Uwanja wa Kigali Arena.

Mbali na Kungfu, michezo mingine ikiwemo taekwondo, karate, judo na ndondi pia imeoneshwa na mashirikisho mbalimbali.

Mwenyekiti wa shirikisho hili Marc Uwiragiye amesisitiza kuwa maonesho hayo ni muhimu sana kwa Wanyarwanda na hawana budi kuonesha kwa dunia kuwa wako pamoja ili kukuza maendeleo endelevu kupitia sanaa ya Kungfu.

Kwa mujibu wa Uwiragie, wachezaji kutoka shule mbalimbali nchini Rwanda wamefanya mazoezi kwa wiki mbili kabla ya maonesho hayo.    

Shirikisho hilo lenye klabu 31 kote nchini Rwanda zikiwemo 14 kutoka mji mkuu Kigali, na wanachama 4,000 wakiwa na wachezaji 2,500, lilianzishwa mwaka 2007, na linalenga kukuza mawasiliano ya kitamaduni na urafiki kati ya China na Rwanda.