Watu wawili wafariki na wengine 17 kujeruhiwa katika ajali ya barabarani, Tanzania
2022-03-21 14:06:14| CRI

Watu wawili wamefariki dunia na wengine 17 kujeruhiwa jana alfajiri baada ya basi dogo lililokuwa likitembea kugongana na lori lililosimama katika mkoa wa Morogoro, Tanzania.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Morogoro Fortunatus Musilimu amesema ajali hiyo ilitokea katika eneo la Nane Nane lililoko barabara kati ya Dar es Salaam na Dodoma. Basi hilo lililogongana na lori lilikuwa linatoka Mbezi, Dar es Salaam kwenda Dodoma. Watu wawili wote wanaume walifariki wakati wanapatiwa matibabu kwenye hospitali ya mkoa wa Morogoro, na kwamba watu watatu kati ya 17 waliojeruhiwa wapo mahututi.

Kabla ya ajali hii, usiku wa Ijumaa iliyopita ilitokea ajali nyingine katika mkoa wa Morogoro, ambapo basi moja liligongana uso kwa uso na lori katika kijiji cha Melela Kibaoni, na watu 23 walifariki.