Ripoti ya UM yasema ukosefu wa usalama wa maji katika Afrika watishia ajenda ya maendeleo endelevu
2022-03-22 09:48:05| CRI

Ripoti ya UM yasema ukosefu wa usalama wa maji katika Afrika watishia ajenda ya maendeleo endelevu_fororder_3

Juhudi za Afrika za ukuaji jumuishi, uvumilivu wa hali ya hewa na utulivu vipo hatarini kutokana na usalama wa maji kuwa hatarini barani humo.

Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyopewa jina la “Usalama wa Maji katika Afrika: Tathmini ya Awali” iliyotolewa mjini Nairobi kufuatia Siku ya Maji Duniani ambayo ni leo Jumanne. Ripoti hiyo imebainisha kuwa upatikanaji wa maji salama ya kunywa na shughuli za msingi za usafi zinaendelea kuwa adimu kwa watu barani humo, kwani kiwango cha usalama wa maji kwa ujumla kiko chini sana.

Ripoti hiyo iliyojumuisha nchi 54 za Afrika, imetathmini viashiria 10 na kusema kwamba takriban watu milioni 500 katika nchi 19 barani humo wana tatizo la maji. Nchi 13 tu kati ya 54 ndio zina usalama wa maji kwa kiwango cha wastani katika miaka mitano iliyopita, huku theluthi moja zikiwa na kiwango cha chini ya asilimia 45 cha usalama wa maji duniani.