Kenya yalenga kuwachanja watu wazima milioni 19 dhidi ya COVID-19 hadi ifikapo Juni
2022-03-22 09:51:50| CRI

Wizara ya Afya ya Kenya imesema hadi sasa nchi hiyo imewachanja watu wazima milioni 15.9 dhidi ya COVID-19, na kuiweka nchi kwenye njia ya kufikia lengo lake la kuchanja kikamilifu asilimia 70 ya watu wazima hadi ifikapo Juni.

Kulingana na wizara hiyo, watu milioni 7.9 wamechanjwa kikamilifu dozi zote mbili. Kenya inapanga kuchanja kikamilifu watu wazima milioni 19 itakapofika katikati ya mwaka huu na watu wazima wote milioni 27 ifikapo mwisho wa mwaka.

Wizara hiyo ilisema katika taarifa yake kuwa chanjo hizo milioni 7.9 zinamaanisha kuwa taifa hilo limefikia asilimia 42 ya lengo lake la kuwachanja watu wazima milioni 19.

Kenya kufikia sasa imepokea dozi milioni 27 za chanjo ambazo ni Moderna, AstraZeneca, Pfizer, Johnson & Johnson na Sinopharm.