Watu 34 wauawa kwenye mashambulizi kaskazini mwa Nigeria
2022-03-23 10:50:53| CRI

Takriban watu 34 waliuawa kufuatia mashambulizi yaliyoratibiwa na watu wenye silaha waliovamia vijiji vinne katika jimbo la Kaduna, kaskazini magharibi mwa Nigeria siku ya Jumapili.

Kamishna wa usalama na maswala ya ndani ya jimbo hilo Samuel Aruwan aliwaambia waandishi wa habari kuwa watu saba pia walijeruhiwa wakati zaidi ya nyumba 200 na maduka 32 yalichomwa moto wakati wa mashambulizi ya Jumapili usiku kwenye vijiji vya Tsonje, Agban, Katanga na Kadarko katika eneo la serikali ya mtaa wa Kaura huko Kaduna.

Aruwan alisema magari matatu na pikipiki 17 pia ziliharibiwa na watu wenye silaha, na sababu za mashambulizi hayo bado hazijajulikana.