Tanzania yatangaza wiki ya kuwasaka wahamiaji haramu nchi nzima
2022-03-23 10:43:55| CRI

Mamlaka ya Uhamiaji Tanzania jana Jumanne ilitangaza wiki ya msako wa wahamiaji haramu katika nchi nzima.

Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji Tanzania Dkt Anna Makakala amewaambia wanahabari huko Morogoro kuwa askari wa uhamiaji watatafuta kila pembe ili kuwapata wahamiaji hao haramu. Makakala amewaonya Watanzania kutojihusisha na biashara ya magendo ya binadamu, na kusema wahalifu watachukuliwa sheria kali.

Amebainisha kuwa mamlaka ya uhamiaji imepata idhini ya kuajiri maafisa wapya wa uhamiaji ambao watakuwa na jukumu kubwa katika msako wa wahamiaji haramu katika siku za baadaye.