Malawi yasaini Hati ya Maelewano na China juu ya ushirikiano wa Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”
2022-03-24 10:50:12| CRI

Malawi jana ilisaini Hati ya Maelewano na China juu ya ushirikiano wa Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” huko mjini Lilongwe, ambapo imekuwa nchi mpya kujiunga na mradi huo.

Waziri wa mambo ya nje wa Malawi Bibi Nancy Tembo akihudhuria hafla ya kutia saini amesema, kujiunga na Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” kutatia nguvu mpya kwa ushirikiano kati ya nchi mbili. Serikali ya Malawi inajitahidi kuendelea kuimarisha uhusiano na China kwenye masuala yenye maslahi ya pamoja. Ametoa wito wa kuimarisha ushirikiano wa pande mbili katika sekta za kupunguza umaskini, kilimo, miundombinu, afya na nyinginezo.

Kwa upande wa balozi wa China nchini Malawi Bw. Liu Hongyang amesema China inapenda kuunganisha Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” na Ajenda ya mwaka 2063 ya Malawi, na kutoa mchango kwa nchi hiyo katika ujenzi wa nchi yenye ustawi wa pamoja na uwezo wa kujitegemea.