Tanzania yaboresha utoaji wa tahadhari ya mapema wakati wa maafa ya hali ya hewa
2022-03-24 10:55:27| CRI

Tanzania imefanya juhudi kubwa za kuimarisha utoaji wa tahadhari ya mapema nchini ili kupunguza maafa ya hali ya hewa.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Makame Mbarawa akitoa taarifa ya kuadhimisha Siku ya Hali ya Hewa Duniani alisema, juhudi hizi ni pamoja na kuimarisha utoaji wa tahadhari ya mapema ya hali ya hewa kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).

Amesema utabiri wa hali ya hewa na huduma zinazotolewa na TMA zimeinuliwa kwa kiwango kikubwa katika ubora na usahihi, ambapo katika misimu ya hivi karibuni usahihi wa utabiri wa hali ya hewa ni kati ya asilimia 93 na asilimia 96.

Mbarawa amesema kiwango hicho kimezidi kile cha chini ya usahihi wa asilimia 70 kinachopendekezwa na Shirika la Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani (WMO).