Idadi ya vifo kutokana na mashambulizi ya Somalia yaongezeka hadi 48
2022-03-25 10:12:15| CRI

Idadi ya vifo kutokana na mashambulizi ya Somalia yaongezeka hadi 48_fororder_4

Idadi ya vifo kutokana na mashambulizi ya kujitoa mhanga yaliyofanyika Jumatano katika mji wa kati wa Somalia wa Beledweyne imeongezeka hadi 48 huku wengine 108 wakijeruhiwa.

Mkuu wa Jimbo la Hirshabelle nchini Somalia Ali Gulawe Hussein alisema idadi hiyo inaweza kuendelea kuongezeka kwani watu kadhaa waliojeruhiwa wako katika hali mbaya.

Hussein alitoa wito kwa polisi kuimarisha usalama katika kambi ya kijeshi ya Lamagalaay ambako uchaguzi wa baraza la chini unafanyika, takriban kilomita 300 kaskazini mwa mji mkuu wa Somalia, Mogadishu. Alisema kundi la wapiganaji wa Al-Shabab ni adui wa watu wa Somalia na walilenga watu mashuhuri katika jamii, akitaka vikosi vya usalama kufanya uchunguzi wa kina kuhusu mashambulizi hayo.

Miongoni mwa waliouawa katika mashambulizi hayo ni pamoja na mbunge mwanamke Amina Mohamed ambaye aliuawa alipokuwa akikaribia kituo cha kupigia kura mjini humo.