UM na wasimamizi wa amani watoa wito wa kusimamisha mapambano nchini Sudan Kusini
2022-03-25 10:11:05| CRI

Umoja wa Mataifa na wasimamizi wa amani wa Sudan Kusini wametoa wito kwa pande zinazohusika za mgogoro kusimamisha mapambano kwenye eneo la Upper Nile ambalo lina utajiri wa mafuta, na kufanya mazungumzo ili kusaidia kutatua tofauti zitakazoweza kutishia mapatano hafifu ya amani.

Katika taarifa tofauti, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS) na tume iliyoundwa upya ya Usimamizi na Tathmini ya Pamoja (RJMEC) zimezitaka pande zote kuzingatia kwa pande zote makubaliano ya amani.

Mkuu wa UNMISS Nicholas Haysom alisema uamuzi wa chama cha upinzani cha Sudan People’s Liberation-In Opposition (SPLM-IO) kusimamisha ushiriki wake katika mifumo ya usalama ya makubaliano ya amani unatia wasiwasi mkubwa.

Alisema hata hivyo, wanatambua wasiwasi unaoletwa na SPLM-IO, hasa ongezeko la tishio la mapambano kwenye Majimbo ya Upper Nile na Unity, ambalo limeathiri moja kwa moja makazi yao pamoja na raia.”