Ofisa wa Sudan Kusini ahimiza pande mbalimbali za Sudan kufanya mazungumzo ili kutimiza utulivu
2022-03-28 09:04:52| CRI

Ofisa wa serikali kutoka Sudan Kusini ametoa wito mazungumzo kati ya pande mbalimbali za kisiasa za Sudan na vikosi vya taifa ili kufikia makubaliano kwa ajili ya utulivu wa nchi hiyo.

Kwenye mkutano kati yake na mkuu wa Baraza la Mamlaka la Mpito la Sudan Abdel Fattah Al-Burhan, mshauri wa rais wa Sudan Kusini anayeshughulikia mambo ya usalama Bw. Tut Gatluak, amesema utulivu na usalama wa Sudan utanufaisha utulivu na usalama nchini Sudan Kusini na katika kanda nzima.

Bw. Gatluak amesema mkutano umepitia hali ya kisiasa ya hivi sasa nchini Sudan na juhudi za serikali ya Sudan, Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kutafuta njia ya kutatua hali ya sasa nchini Sudan.

Tangu Oktoba 25 mwaka jana, mkuu wa Jeshi la Sudan Abdel Fattah Al-Burhan alitangza hali ya dharura na kuvunja baraza la mamlaka na serikali, na kuifanya Sudan iingie katika msukosuko wa kisiasa.