UNHCR yasema hali ya usalama kaskazini mwa Ethiopia bado tete
2022-03-29 08:46:31| CRI

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limesema hali ya kibinadamu kwenye sehemu ya kaskazini ya Ethiopia bado ni tete.

Katika ripoti yake mpya ya dharura, shirika hilo limesema hali ya kibinadamu kaskazini mwa Ethiopia inatia wasiwasi, ambako kuna wakimbizi wa ndani milioni 2.6, watu laki 2.4 waliorejea nchini, pamoja na wakimbizi na wanaotafuta hifadhi elfu 94 kwenye maeneo ya Afar, Amhara na Tigray.

Kwa mujibu wa UNHCR, mahitaji ya kibinadamu yameongezeka kwa kiasi kikubwa, huku zaidi ya watu milioni 9.4 wakihitaji msaada wa dharura wa chakula na misaada mingine.