DRC yalishutumu jeshi la Rwanda kuunga mkono mashambulizi ya waasi dhidi ya vituo vya jeshi lake
2022-03-29 08:47:06| CRI

Msemaji wa Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (FARDC) amesema, askari wawili wa Rwanda walikamatwa na kushutumiwa kuunga mkono waasi wa Kundi la M23 kwenye mashambulizi waliyoyafanya mapema jumatatu dhidi ya vituo vya kijeshi vilivyoko Rutshuru, kaskazini ya Goma, ambao ni mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini.

Msemaji wa Gavana wa mkoa wa Kivu Kaskazini Jenerali Sylvain Ekenge, amethibitisha kuwa askari wawili wa jeshi la Rwanda walikamatwa kwenye mashambulizi hayo, na ameishutumu Rwanda kushirikiana na waasi wa kundi la M23.