Ujumbe wa Ukraine na Russia wawasili nchini Uturuki kwa ajili ya mazungumzo ya amani
2022-03-29 08:59:36| CRI

Ujumbe wa Ukraine na Russia umewasili nchini Uturuki kwa ajili ya mazungumzo ya ana kwa ana yenye lengo la kutafuta amani, yakileta kufikia maendeleo makubwa kukomesha mgogoro.

Rais Tayyip Erdogan wa Uturuki anatarajiwa kuhutubia wajumbe wa pande mbili kabla ya kuanza kwa mazungumzo yanayotarajiwa kuanza saa nne na nusu asubuhi kwa saa za Uturuki.

Jumapili kwenye mazungumzo kwa njia ya simu na mwenzake wa Russia Vladimir Putin, Rais Erdogan alimwambia kusimamisha mapigano na amani ni lazima vipatikane haraka iwezekanavyo, na hali ya kibinadamu ni lazima iboreshwe haraka.

Rais Erdogan pia amesisitiza kuwa Uturuki itaendelea kufanya kila inaloweza kutafuta amani kati ya pande hizo mbili.