WFP yasema msaada wa chakula wa China umewafikia maelfu ya waathirika wa ukame nchini Uganda
2022-03-30 08:42:28| CRI

Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa WFP limesema msaada wa chakula uliotolewa na China kupitia shirika hilo umewafikia maelfu ya waathirika wa ukame, wakiwemo watoto, kaskazini mashariki mwa Uganda.

Kwenye halfa ya kusaini makabidhiano, mwakilishi wa WFP nchini Uganda Bw. Abdirahman Meygag, amesema msaada huo uliotolewa na China mwaka jana umewafikia watoto zaidi ya laki 1.3 kupitia mpango wa lishe shuleni na wengine elfu 70 kupitia msaada wa chakula unaolenga kuboresha usalama wa chakula katika familia zilizo hatarini.

Balozi wa China nchini Uganda Bw. Zhang Lizhong, amesema mbali na msaada, China inajadili na upande wa Uganda kutafuta namna ya kuisaidia Uganda kutumia kilimo katika kupambana na umaskini.

Abdirahman Meygag (L), UN World Food Program (WFP) representative to Uganda, and Zhang Lizhong, Chinese ambassador to Uganda, attend a handover certificate signing ceremony in Kampala, Uganda, on March 29, 2022. 

Mwakilishi wa WFP nchini Uganda (kushoto) Abdirahman Meygag, na Balozi wa China nchini Uganda Zhang Lizhong wakishiriki kwenye  hafla ya kutia saini na kukabidhiana nyaraka za makubaliano  huko Kampala, Uganda, Machi 9, 2022.