Kenya yasema watoto 754,906 wanahitaji matibabu kutokana na utapiamlo mkali
2022-03-30 09:28:55| CRI

Afisa wa serikali ya Kenya amesema watoto 754,906 wenye umri chini ya miaka mitano, wajawazito na kina mama wanaonyonyesha 103,286 wanahitaji matibabu ya utapiamlo mkali kutokana na ukame unaoendelea nchini humo.

Mkurugenzi mkuu wa wizara ya afya ya Kenya Bw. Patrick Amoth, amesema mjini Nairobi kuwa serikali imeanzisha hatua za kukabiliana na tatizo hilo ikiwemo usambazaji wa bidhaa za kuokoa maisha na ukaguzi wa lishe.

Bw. Amoth ameongeza kuwa utapiamlo ni chanzo kikuu kwa watoto kupata magonjwa, kufariki na kulazwa hospitali, hali inayohitaji uingiliaji wa haraka.