Msumbiji yaitisha mkutano wa baraza la biashara la taifa baada ya kusimamishwa kwa miaka miwili
2022-03-31 09:19:00| CRI

Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji amefungua Mkutano wa Sekta ya Binafsi wa Mwaka CASP, ambao ni jukwaa kubwa zaidi la biashara la mazungumzo kati ya sekta za umma na binafsi nchini humo.

Mkutano huo utakaodumu kwa siku tatu ukiwa ni wa awamu ya 17 baada ya kusimamishwa kwa miaka 2 kutokana na janga la Corona, umefanyika kwa njia ya ana kwa ana na mtandao wa Internet ukiwa na sehemu tatu ambazo ni kuhimiza mazungumzo kati ya sekta ya umma na sekta binafsi, mkutano wa uwekezaji na vyumba vya biashara.

Shirikisho la Uchumi la Msumbiji CTA limetoa taarifa ikisema, jumla ya dola milioni 990 za kimarekani kutoka miradi 50 kutoka sekta za kilimo, nishati, utalii na miundombinu zitakuwepo katika mkutano huo.