Sudan yawaachilia wageni 18 kutoka kwa wasafirishaji haramu wa binadamu
2022-04-01 09:32:14| CRI

Idara ya Ujasusi ya Sudan (GIS) jana iliwaachilia huru wageni 18 walioshikiliwa na kundi la wasafirishaji haramu wa binadamu katika jimbo la Gadaref mashariki mwa Sudan.

Mkuu wa Idara hiyo katika jimbo la Gadaref Bw. Adam Osman alisema kuwa idara hiyo katika jimbo la Gadaref ilifanikiwa kuzuia biashara haramu ya binadamu na kuwaachia raia 18 wa Ethiopia katika eneo la Galanahal.

Ametoa wito kwa mashirika ya kimataifa hususan shirika la wahamiaji la kimataifa kuiunga mkono Sudan kukabiliana na uhamiaji haramu.