Mjumbe wa China asisitiza kuendelea kuiunga mkono Somalia katika sekta ya usalama
2022-04-01 09:32:51| CRI

Naibu balozi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Dai Bing, jana alisema jumuiya ya kimataifa inapaswa kuendelea kutoa misaada kwa Somalia katika sekta ya usalama.

Hivi sasa hali ya usalama nchini Somalia bado inakabiliwa na changamoto, baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio la kuunda upya kwa tume ya kulinda amani ya Umoja wa Afrika nchini Somalia katika tume ya mpito ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS).

Bw. Dai Bing alisema China inaunga mkono uamuzi wa Baraza la Usalama kuhusu kuiunga mkono ATMIS na kuzitaka pande husika ziimarishe uratibu katika mchakato wa utekelezaji wa operesheni na kushirikiana na serikali ya Somalia, na kuisaidia kuchukua jukumu la msingi la kulinda usalama wa taifa hatua kwa hatua.