Kiongozi wa Sudan ataka tume ya Umoja wa Mataifa isiwe na upendeleo katika mgogoro wa kisiasa nchini humo
2022-04-04 08:31:56| CRI

Kiongozi wa Sudan ataka tume ya Umoja wa Mataifa isiwe na upendeleo katika mgogoro wa kisiasa nchini humo_fororder_Chairman_of_the_Sovereignty_Council_of_Sudan_Abdel_Fattah_Abdelrahman_Burhan_in_October_2019_(cropped)

Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Mpito nchini Sudan, Abdel Fattah Al-Burhan ametoa wito kwa Tume ya Umoja wa Mataifa nchini humo (UNITAMS) kuweka umbali sawa kwa pande zote wakati mgogoro wa kisiasa ukiendelea nchini humo.

Al-Burhan amesema hayo jana jumapili walipokutana na mkuu wa Tume hiyo Volker Perthes katika mji mkuu wa Sudan, Kahrtoum.

Taarifa iliyotolewa na Baraza hilo imemnukuu Al-Burhan akisema, mazungumzo hayo hayakuhusisha mambo yote yanayoendelea nchini humo, na pia hayakujumuisha viashiria chanya vilivyotokea.

Kwa upande wake, Perthes amesema mazungumzo hayo yalitokana na taarifa na ripoti zilizoandaliwa na ofisi yake mjini Khartoum, lakini alieleza utayari wake wa kutathmini taarifa yoyote isiyo sahihi iliyojumuishwa kwenye ripoti iliyowasilishwa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.