Chama kikuu cha upinzani nchini Sudan Kusini chajiunga tena na utaratibu wa usalama
2022-04-05 08:37:59| CRI

Chama kikuu cha upinzani nchini Sudan Kusini, SPLM/A-IO kimekubali kuendelea kushiriki kwenye utaratibu wa usalama baada ya kujitoa hivi karibuni kutokana na mashambulizi yasiyo na sababu katika vituo vyake.

Uamuzi huo ulitangazwa jumapili mjini Juba, na kiongozi wa Chama hicho ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Sudan Kusini, Riek Machar.

Uamuzi huo umetokana na ziara iliyofanywa na makamu mwenyekiti wa Baraza la Mpito la Utawala la Sudan, Mohamed Hamdan Daqlu, ambaye alifanya mazungumzo na rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na pande nyingine zilizosaini makubaliano ya amani ya mwaka 2018.