Mahakama nchini Rwanda yathibitia hukumu ya kifungo cha miaka 25 kwa Paul Rusesabagina
2022-04-05 08:36:53| CRI

Mahakama mjini Kigali, Rwanda, imethibitisha hukumu ya kifungo cha miaka 25 jela iliyotolewa kwa Paul Rusesabagina, mmiliki wa hoteli ambaye katika filamu inayoitwa ‘Hotel Rwanda’ alionyeshwa kama shujaa.

Mwezi Septemba mwaka jana, Rusesabagina alikutwa na makosa manane yanayohusiana na vitendo vya kigaidi vilivyofanywa na kundi la FLN mwaka 2018, vilivyosababisha vifo vya raia tisa wa Rwanda katika eneo la kusini magharibi kwa nchi hiyo.

Upande wa mashtaka ulikata rufaa dhidi ya adhabu hiyo kwa msingi kuwa mahakama ya chini umetoa adhabu ndogo kwa mshtakiwa huyo, lakini hata hivyo, jana jumatatu, mahakama ya rufaa chini ya Jaji Francois Regis ilisema hakuna sababu ya kuongeza adhabu hiyo.