Watu 7 wafariki katika ajali ya treni nchini DRC
2022-04-05 09:21:11| CRI

Watu 7 wamefariki na wengine 14 kujeruhiwa katika ajali ya treni ya mizigo kusini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Habari zilizotolewa na Wizara ya Uchukuzi ya nchi hiyo zinasema, mabehewa matatu kati ya manane ya treni hiyo yaliacha njia saa 1 usiku kwa saa za huko katika sehemu ya Lubudi mkoani Lualaba.

Waziri wa Uchukuzi wa nchi hiyo Okende Cherubin ameahidi kuunda timu huru kuchunguza ajali hiyo.

Ajali za treni zimetokea mara kwa mara nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kutokana na hali mbaya ya treni na uchakavu wa reli.