Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali wachunguza ripoti za vifo vya raia
2022-04-05 08:29:39| CRI

Naibu msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Farhan Haq jana amesema Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali unachunguza ripoti za raia waliouawa kwenye mapigano yaliyotokea wiki iliyopita kati ya wanajeshi wa serikali na vikundi vya wapiganaji.

Ripoti zilizotolewa zinatofautiana kuhusu idadi ya vifo vya raia, lakini zinakubali kwamba idadi hiyo ni kubwa, na pia ripoti hizo zinasema, jeshi la Mali lilipambana na wapiganaji wanaoaminika kuwa na uhusiano na kundi la IS au al Qaeda.

Bw. Haq amesema, Umoja huo unafanya kazi ili kuthibitisha ukweli wa tukio hilo, ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu.