Watu milioni 18 kuingia kwenye ukosefu wa chakula nchini Sudan kutokana na mgogoro wa uchumi na uhaba wa mvua
2022-04-06 09:04:28| CRI

Watu milioni 18 kuingia kwenye ukosefu wa chakula nchini Sudan kutokana na mgogoro wa uchumi na uhaba wa mvua_fororder_f31fbe096b63f6244807c8e2031537f11b4ca350

Naibu msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq jana amesema, msukosuko wa uchumi na uhaba wa mvua vimeongeza mahitaji ya kibinadamu nchini Sudan kwenye viwango visivyoshuhudiwa, ambapo watu milioni 18 wako hatarini kukabiliwa na ukosefu mkubwa wa chakula.

Faq amesema kuwa, Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja huo (FAO), zinakadiria idadi ya watu nchini Sudan wanaokabiliwa na ukosefu wa chakula kuongezeka karibu mara mbili itakapofika mwezi Septemba.

Mwaka jana watu milioni 9.8 nchini Sudan walikabiliwa na ukosefu wa chakula, na watu karibu milioni 18 wanatishiwa kuingia hali hiyo kufikia mwezi Septemba.