Rais wa Angola ashiriki uzinduzi wa miradi muhimu iliyojengwa na kampuni ya China
2022-04-06 08:37:48| CRI

Rais wa Angola Bw. Joao Lourenco ameshiriki kwenye uzinduzi wa awamu ya kwanza ya mradi wa kukabiliana na ukame katika mkoa wa Cunene uliotekelezwa na kampuni ya China.

Rais Lourenço amesema, kukamilika kwa mradi huo kutaboresha sana hali ya wakaazi wa eneo hilo wanaokumbwa na ukame, na pia utaweka mazingira mazuri kwa maendeleo ya kilimo nchini humo.

Habari zinasema, kampuni ya China ilitoa ajira kwa idadi kubwa ya wenyeji katika ujenzi wa mradi huo.

Awamu ya kwanza ya mradi huo ni pamoja na njia ya maji yenye urefu wa kilomita 150 inayounganisha mto Cunene, mabwawa, vituo vya maji na vifaa vingine.