EAC kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 28 ya mauaji ya kimbari ya Rwanda
2022-04-06 08:34:30| CRI

Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imearifu kuwa, inafanya maandalizi ya kumbukumbu ya miaka 28 ya Mauaji ya Kimbari yaliyotokea mwaka 1994 dhidi ya Watutsi nchini Rwanda tarehe 7 mwezi huu.

Taarifa iliyotolewa na Jumuiya hiyo imesema, maadhimisho hayo yatafanyika katika makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki mjini Arusha, kaskazini mwa Tanzania.

Taarifa hiyo imesema EAC itaungana na washirika wengine katika kuadhimisha kumbukumbu hiyo, zikiwemo mamlaka za serikali ya mkoa wa Arusha, jamii za Wanyarwanda walioko Arusha na Kilimanjaro, Ubalozi wa Rwanda nchini Tanzania na Ofisi ya Mfumo wa Kimataifa wa Kushughulikia Mabaki ya Kesi za Mauaji ya Kimbari (IRMCT).