Wataalamu wa Afrika wasema ufadhili wa ndani ni muhimu katika kutimiza lengo la kupunguza uchafuzi wa hewa
2022-04-06 08:49:00| CRI

Wanasayansi barani Afrika wamesema, ukusanyaji wa rasilimali za ndani ni muhimu katika kutimiza juhudi za kupunguza utoaji wa hewa chafu katika bara hilo ambalo madhara ya mabadiliko ya tabianchi yameongezeka.

Akizungumza katika mkutano kwa njia ya video uliofanyika jijini Nairobi, Kenya, mtaalamu wa masuala ya ufadhili wa hali ya hewa kutoka nchini Zimbabwe, Nokuthula Dube amesema, kutokana na uungaji mkono usio wa uhakika kutoka nje, nchi za Afrika zinapaswa kutumia masoko ya mitaji ya ndani kufadhili utekelezaji wa ajenda yao ya kupunguza utoaji wa hewa ya carbon.

Naye mtaalamu wa hali ya hewa na nishati kutoka Afrika Kusini, Brett Cohen amesema, sekta binafsi zinapaswa kuwezeshwa ili kuchochea uwekezaji katika nishati safi, usafiri unaotoa uchafuzi mdogo na kilimo kinachovumilia mabadiliko ya tabianchi.