Aliyekuwa rais wa Burkina Faso Bw. Roch Marc Christian Kabore aruhusiwa kurudi nyumbani kwake
2022-04-07 08:16:44| CRI

Serikali ya mpito ya Burkina Faso imetangaza kuwa, rais wa zamani wa nchi hiyo Bw. Roch Marc Christian Kabore, aliyekamatwa tarehe 24, Januari wakati wa mapinduzi ya kijeshi yaliyompindua, ameruhusiwa kurejea nyumbani kwake.

Taarifa iliyotolewa jana na serikali hiyo imesema, Bw. Kabore atarejea katika makazi yake katika mji mkuu wa nchi hiyo, Ouagadougou, huku hatua zikichukuliwa kuhakikisha usalama wake.