Baraza la Biashara la Afika Mashariki laangazia soko la kikanda ili kuchochea ukuaji wa uchumi
2022-04-07 08:37:32| CRI

Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC) litaongeza fursa zinazotokana na Eneo la Biashara Huria la Afrika (AfCFTA) ili kuchochea uwekezaji, ukuaji, na ufufukaji baada ya janga la COVID-19.

Akizungumza katika mkutano ulioandaliwa kwa pamoja na Baraza hilo pamoja na Kamati ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa (UNECA) uliofanyika kwa njia ya video jijini Nairobi, Kenya hapo jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza hilo John Bosco Kalisa amesema, kanda hiyo inaweza kufaidika na kuanzishwa kwa soko lisilo na mipaka la bara la Afrika, kuwa na usawa katika ushuru, kuondoa vizuizi vya kibiashara, na kushiriki zaidi katika biashara kwa njia ya kidijitali.

Ameongeza kuwa, faida zinazoweza kupatikana ni pamoja na kuongezeka kwa biashara ya kuvuka mpaka, uwekezaji, ajira, kuongeza thamani ya bidhaa, ushindani katika sekta binafsi, uvumbuzi na uhamishaji wa teknolojia.