WHO yasema theluthi mbili ya watu barani Afrika waambukizwa na COVID-19
2022-04-08 08:53:52| CRI

WHO yasema theluthi mbili ya watu barani Afrika waambukizwa na COVID-19_fororder_Matshidiso_Rebecca_Moeti

Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) tawi la Afrika Matshidiso Moeti amesema, huenda theluthi mbili ya watu barani Afrika wameambukizwa na COVID-19.

Moeti amenukuu ripoti ya Shirika hilo, akisema idadi halisi ya watu walioambukizwa virusi vya Corona inaweza kuwa mara 97 ya kesi zilizoripotiwa barani Afrika, ikimaanisha kuwa theluthi mbili ya watu barani humo wameambukizwa au waliwahi kuambukizwa virusi hivyo.

Moeti amesema ripoti hiyo imethibitisha kuwa maambukizi ya virusi vya Corona bado yanaendelea, na kuna uwezekano wa kutokea kwa aina mpya ya virusi vya hatari zaidi. Amesisitiza tena umuhimu wa chanjo, na kuzihimiza nchi za Afrika kuharakisha mchakato wa kuchanja watu.

Takwimu zilizotolewa na WHO zinaonesha kuwa, hadi sasa Afrika imeripoti kesi milioni 1.15 za maambukizi ya COVID-19, na vifo laki 2.5 kutokana na virusi hivyo.