Chama cha MPP cha nchini Burkina Faso chasema rais wa zamani wa nchi hiyo hana uhuru kamili
2022-04-08 08:46:37| CRI

Chama cha MPP cha aliyekuwa rais wa zamani wa Burkina Faso Roch Marc Christian Kabore aliyeruhusiwa kurejea kwenye makazi yake jumatano wiki hii kimesema, rais huyo hana uhuru kamili.

Taarifa iliyotolewa na Chama hicho imesema, uhuru wa rais huyo wa zamani bado unakabiliwa na vikwazo, na kuitaka serikali ya mpito kuondoa mahitaji mbalimbali yaliyowekwa na kumwachia Bw. Kabore bila ya masharti yoyote.