Watu 8 wauawa kwenye mlipuko nchini DRC
2022-04-08 08:31:43| CRI

Gavana wa mkoa wa Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Bw. Constant Ndima Kongba amethibitisha kuwa, watu wanane wameuawa kwenye mlipuko uliotokea jana jioni kwenye baa moja huko Goma, mji mkuu wa mkoa huu.

Waziri wa habari wa DRC ambaye pia ni msemaji wa serikali Bw. Patrick Muyaya amesema kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa, serikali imeanza kufanya uchunguzi kujua chanzo cha mlipuko huo, huku kukiwa na taarifa kuwa huenda mlipuko ulisababishwa na guruneti la askari mmoja wa jeshi la Congo.