Umoja wa Mataifa waongeza msaada wa kibinadamu ili kukwepa njaa nchini Somalia
2022-04-08 08:45:14| CRI

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulika na Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema, inaongeza msaada wake ili kusaidia watu milioni 4.9 walio hatarini zaidi kuathiriwa na ukame nchini Somalia.

Mwakilishi mkazi na mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Adam Abdelmoula amesema, ngazi za mahitaji zinaongezeka kwa kasi kuzidi uwezo na rasilimali zilizopo, na kuonya kuwa hali inaweza kuwa mbaya zaidi itakapofika mwezi Juni.

Kwa mujibu wa ripoti kuhusu hali ya ukame iliyotolewa hivi karibuni na Ofisi hiyo, hali ya ukame nchini Somalia imezidi kuwa mbaya na kuifanya nchi hiyo kukabiliwa na hatari ya kukumbwa na baa la njaa.