Polisi ya Kenya yamkamata mtu anayetuhumiwa kuchunguza barabara ya mwendo kasi jijini Nairobi
2022-04-11 09:53:40| cri

Polisi ya Kenya jana Jumapili ilithibitisha kuwa inamhoji mtuhumiwa wa ugaidi ambaye alipatikana akichunguza barabara mpya ya mwendo kasi “Nairobi Expressway”.

Kwa mujibu wa ripoti ya usalama, mtuhumiwa huyo, anayetambulika kama David Mulinge Kasimbi, alipatikana katika sehemu ambayo hawapaswi kupita watembea kwa miguu, na kwamba wakati alipohojiwa alishindwa kutoa majibu ya kuridhisha. Polisi imesema baadhi ya sehemu za barabara haziruhusiwi kufikiwa na watembea kwa miguu na zinalindwa na maafisa wa usalama.

Mtu huyo amekamatwa wakati ambao usalama umeimarishwa kufuatia ripoti kwamba al-Shabaab wamepeleka idadi isiyojulikana ya watu wa kujitoa muhanga kufanya mashambulizi ya kigaidi nchini Kenya.