Mkutano wa Kwanza wa Mazungumzo ya Ustaarabu kati ya China na Afrika wafanyika
2022-04-11 09:55:05| cri

Mkutano wa Kwanza wa Mazungumzo ya Ustaarabu kati ya China na Afrika wafanyika_fororder_43a7d933c895d143ff3d9bc75681a8085baf0701

Mkutano wa Kwanza wa Mazungumzo ya Ustaarabu kati ya China na Afrika unaoandaliwa na  Taasisi ya Sayansi ya Jamii ya  China, na kuendeshwa na Taasisi ya Utafiti wa Mambo ya Afrika ya China na Ofisi ya Umoja wa Afrika nchini China, ulifanyika Aprili 9 mtandaoni na nje ya mtandao.

Mkutano huo wenye maudhui ya “mazungumzo ya ustaarabu yahimiza ujenzi wa Jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya”, unalenga kuandaa jukwaa jipya la mawasiliano ya utamaduni kati ya China na Afrika, kupanua mawasiliano kama hayo, na kuchangia busara na nguvu katika kujenga Jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya na Jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

Mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Umoja wa Afrika nchini China Rahamtalla M. Osman akihutubia mkutano huo alisema, ustaarabu wa jadi wa Afrika na wa China, zinajumuisha kutoa kipaumbele maslahi ya pamoja, na kuishi pamoja kwa masikilizano kwa binadamu, na kati ya binadamu na mazingira ya asili, mambo kama hayo yanafupisha umbali kati ya staarabu za pande hizo mbili, na kuyafanya mawasiliano kati ya ustaarabu wa Afrika na wa China kuonesha dalili ya usawa, amani na urafiki.