Kundi la M23 latangaza kuondoka katika vijiji vya kaskazini mashariki mwa DRC
2022-04-11 09:52:34| cri

Kundi la waasi lijulikanalo kama “The March 23 Movement” (M23) jana lilitangaza kuondoka katika vijiji lilivyovitwaa awali katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC.

Tangazo hilo lilitolewa baada ya mapambano makali yaliyofanyika siku kadhaa zilizopita kati jeshi la taifa la DRC na kundi la M23 ambalo lilitwaa baadhi ya maeneo ya Rutshuru mkoani Kivu Kaskazini.

Kundi la M23 lilitoa taarifa likisema limeamua kuondoka tena katika maeneo waliyoyatwaa, ili kuruhusu uongozi wao kufanya mazungumzo ya wazi na yenye ufanisi na serikali ya DRC. Taarifa hiyo pia imesema kundi la M23 kamwe halina nia ya kutwaa maeneo na kuyakalia, madhumuni yao ni kutatua mgogoro kati yao na serikali kwa njia ya amani.