Tume ya Umoja wa Afrika yafunga kambi ya jeshi ili kuwalinda wabunge
2022-04-12 09:03:04| cri

Tume ya Mpito wa Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) imesema kwamba imeweka zuio katika Kambi yake ya Halane, ambayo ni kituo cha jeshi, ili kuhakikisha wabunge wanaapishwa salama siku ya Alhamisi.

ATMIS imesema zuio hilo ni hatua ya tahadhari ambayo tume hiyo imeitumia tangu kuanzishwa kwake mwaka 2007 ili kuzuia majaribio ya magaidi ya kuvunja usalama  kwenye kambi ya msingi , katika nyakati za kuongezeka kwa vitisho vya usalama, sherehe na shughuli nyingine za ngazi ya juu za serikali na washirika wao.

Taarifa iliyotolewa na tume hiyo imesema kuwa madhumuni yake ni kurahisisha operesheni zinazolenga kuhakikisha kwamba Kambi ya Msingi inakuwa salama, na mahali panapofaa katika kipindi hiki muhimu cha shughuli za uchaguzi, zikiwemo sherehe za kuapishwa, sherehe za Miaka 62 ya Jeshi la Somalia na kipindi chote cha Ramadhani.

Kambi ya Halane inatoa makazi kwa maafisa wa ATMIS, Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kimataifa yaliyojitolea kuwahudumia watu wa Somalia.