Sudan yaimarisha usalama kufuatia maandamano ya kuadhimisha miaka mitatu tangu kupinduliwa kwa al-Bashir
2022-04-12 09:02:28| cri

Sudan yaimarisha usalama kufuatia maandamano ya kuadhimisha miaka mitatu tangu kupinduliwa kwa al-Bashir_fororder_苏丹

Mji wa Sudan Khartoum na miji mingine mikubwa iliimarisha usalama jana Jumatatu kutokana na maandamano makubwa yaliyopangwa kufanyika siku hiyo.

Mamlaka za usalama zilifunga madaraja mawili makubwa yanayounganisha Khartoum na miji ya Omdurman na Bahri, na kusambaza jeshi, polisi, na vikosi vya msaada wa haraka kulinda nje ya eneo la majengo ya umma, kama vile Ikulu na Makao Makuu ya Jeshi. Hatua hiyo imechukuliwa kabla ya maandamano hayo ya siku moja yaliyoitishwa na kamati za upinzani na makundi mengine ya wapinzani wa kisiasa ili kuadhimisha siku ya kuondolewa madarakani kwa rais wa zamani wa nchi hiyo Omar al-Bashir Aprili 11, 2019.

Kwenye taarifa yao kamati za upinzani zimesema mandamano ambayo ni ya pili kufanyika Ramadhani, yanalenga kuzuia kurejea kwa chama tawala cha zamani cha NCP na kudai kurejeshwa kwa utawala wa kiraia. Kamati ya Usalama wa Taifa ya Khartoum iliapa kulinda maandamano hayo ya amani lakini ilipiga marufuku mikusanyiko katikati ya Khartoum.