EAC yatangaza kujiandaa kuisaidia DRC kutatua masuala ya kisiasa yanayotokea mara kwa mara
2022-04-13 09:12:19| cri

Jumuiya ya nchi za Afrika Mashairki EAC imetangaza kuwa itawashirikisha watu mashuhuri katika kanda hii ili kutatua migogoro ya kisiasa inayotokea mara kwa mara nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Mpango huu ulitangazwa na katibu mkuu wa EAC, Peter Mathuki, siku chache baada ya DRC kuidhinishwa rasmi kujiunga na jumuiya hiyo yenye nchi wanachama Burundi, Kenya, Rwanda, Sudan Kusini, Tanzania na Uganda.

Mathuki amesema EAC iko katika mchakato wa kuwashirikisha watu mashuhuri, ambao wataisaidia DRC kushughulikia masuala ya amani na usalama, haswa katika eneo la mashariki, na kwamba mpango huo unafuatia agizo la viongozi wa nchi wanachama wa EAC.