Madaktari wa Sudan Kusini waanza kozi ya lugha ya Kichina kwa awamu ya pili
2022-04-13 09:04:25| cri

Madaktari wa Sudan Kusini jana walianza kupata mafunzo ya lugha ya Kichina ya awamu ya pili kwa madhumuni ya kuimarisha maelewano na urafiki kati ya watu wa nchi mbili.

Kwenye hafla ya ufunguzi wa mafunzo iliyofanyika mjini Juba, kansela wa uchumi na biashara katika ubalozi wa China nchini Sudan Kusini Bw. Mu Jianjun amesema lugha ni daraja muhimu la mawasiliano na utamaduni, na hivi sasa lugha ya Kichina inajulikana kote duniani. Darasa hilo la awamu ya pili linaanzishwa kwa ajili ya kuwasaidia madaktari wa Hospitali ya Mafunzo ya Juba waweze kuwasiliana zaidi na kikundi cha madaktari wa China, kufahamu lugha na utamaduni wa China, na kuimarisha maelewano na urafiki kati ya watu wa China na Sudan Kusini.

Mafunzo hayo yalianzishwa mwaka jana na kikundi cha nane cha madaktari wa China, na sasa yanatolewa na kikundi cha tisa.