Kenya yazindua miongozo ya ushirikiano wa kimataifa katika kupambana na ugaidi
2022-04-13 09:08:15| cri

Waendesha mashitaka nchini Kenya jana Jumanne walizindua miongozo ya ushirikiano wa kimataifa katika kupambana na ugaidi na kufadhili ugaidi.

Mkurugenzi wa Ofisi ya Mwendesha Mashataka ya Umma, Noordin Haji amewaambia wanahabari mjini Nairobi kuwa taratibu zinaruhusu mashirika ya ndani kufanya ushirikiano wa kimataifa ili kupata ushahidi, kukabidhi washukiwa na kupata mashahidi wakati wakifanya uchunguzi wa ugaidi.

Amebainisha kuwa miongozo hiyo inaruhusu vyombo vya utekelezaji sheria kufanya mipango ya kujenga uwezo wa kuvuka mipaka, ikilenga kurahisisha kupata maarifa na kuimarisha mahusiano.