Mradi wa kuboresha vyuo vya ufundi vilivyojengwa na China nchini Ghana wapiga jeki elimu ya ufundi nchini humo
2022-04-13 09:07:51| cri

Mradi wa kuboresha vyuo vya ufundi vilivyojengwa na China nchini Ghana umekamilika jana Jumanne, na kuleta msukumo mpya kwenye maendeleo ya elimu ya ufundi nchini humo.

Kwa mujibu wa mkandarasi wa China, Kampuni ya Avic International Holding Corporation, mradi huo ulioanza kujengwa Novemba 2019, unajumuisha jengo la kituo kipya cha mitihani cha Wizara ya Elimu ya Ghana, pamoja na vituo vya mafunzo vya vyuo 15 vya ufundi.

Katika hafla ya kukabidhi iliyofanyika mjini Kumasi, Waziri wa Elimu Yaw Osei Adutwun, kwa niaba ya rais wa Ghana Nana Akufo-Addo ameipongeza serikali ya China kwa kuunga mkono ajenda ya mabadiliko ya elimu ya ufundi ya serikali ya Ghana. Naye balozi wa China nchini Ghana Lu Kun kwenye hotuba yake amesema mradi huo umeonesha maendeleo makubwa katika elimu ya ufundi nchini humo.