Mkuu wa CMG atoa salamu za mwaka mpya
2023-01-01 15:37:14| cri

 

Tarehe mosi Januari 2023, mkuu wa Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) Bwana Shen Haixiong ametoa salamu za mwaka mpya kwa wasikilizaji na watazamaji wote wa CMG walioko nchi za nje.

Marafiki wapendwa,

Wakati tunapokaribisha mwaka mpya wa 2023 wenye matumaini mengi, mimi ninawasalimu kutoka hapa Beijing.

Katika mwaka uliopita, Mkutano Mkuu wa 20 wa Wajumbe Wote wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ulifanyika kwa mafanikio, na kudhihirisha majukumu ya kusukuma mbele Ustawishaji wa Taifa la China kwa pande zote kwa njia ya China ya kutimiza mambo ya kisasa. Ikiwa mshiriki, shahidi na mhabarishaji wa jambo hilo kubwa katika zama mpya, CMG ilitangaza habari kuhusu mkutano huo, na kutoa vipindi mbalimbali vizuri vikiwemo “Uongozi”, “Miaka 10”, ili kufahamisha mambo ya kuvutia ya China katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, na kupongezwa na wasikilizaji na watazamaji wetu wa nchi za nje.

Katika mwaka uliopita, tumetafuta njia ya uvumbuzi inayounganisha mawazo, usanii na teknolojia, ili kutimiza lengo la kutengeneza vipindi bora vingi zaidi. Katika ripoti za Michezo ya Olimpiki ya majira ya Baridi ya Beijing, CMG ilitumia teknolojia za kisasa, ambazo zimeunganisha vizuri moyo wa Olimpiki na utamaduni wa China. Mwenyekiti wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki Bwana Thomas Bach alipongeza ripoti za CMG akisema CMG imefanya kazi kubwa zaidi na kupata mafanikio zaidi katika historia ya Olimpiki. Vipindi vya CMG vya “China kwenye Vitabu vya Kale” na “Mashairi na Michoro ya China” vimeeleza kwa njia ya kisanii sababu ya kuendelea kwa mfululizo kwa ustaarabu wa China, na pia kutafuta njia ya kuendelea kwa pamoja kwa staarabu tofauti za binadamu. Matamasha yaliyoandaliwa na CMG wakati wa Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, Sikukuu ya Mbalamwezi, na Sikukuu ya Mwaka Mpya yameleta njia mpya ya kuelewa utamaduni wa China katika nchi za nje. Maonesho ya filamu yaliyofanywa na CMG barani Latin-Amerika, na Afrika yameanzisha daraja la kuwasiliana kati ya watu na staarabu.   

Katika mwaka uliopita, pia tuliandaa makongamano mbalimbali yakiwemo Kongamano la kwanza la Uvumbuzi wa Vyombo vya Habari Duniani, Kongamano la Mawasiliano ya Watu na Staarabu kati ya China na Argentina, na Kongamano la Ushirikiano wa Vyombo vya Habari kati ya China na Nchi za Kiarabu, ili kuendelea kukuza mfumo wa ushirikiano wa kikanda wa “Wenzi wa Vyombo vya Habari”, na kuongeza urafiki na vyombo vingine vya habari duniani. Baada ya kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC, tuliandaa shughuli 58 za kuwasiliana na vyombo vya habari vya nchi za nje, ili kujadili maana ya zama hii na kimataifa ya njia ya China ya kutimiza mambo ya kisasa, ambazo ziliitikiwa kutangazwa na zaidi ya vyombo 2,000 vya habari duniani.

Rais Xi Jinping wa China alisisitiza mara nyingi kwamba, China ina nia thabiti ya kuwa upande sahihi wa historia, na kuwa maendeleo ya ustaarabu wa binadamu, na inajitahidi kutoa busara na mipango ya China kwa amani na maendeleo ya binadamu. Ushawishi ni kipimo muhimu cha vyombo vya kimataifa vya habari, na ukweli ni uhai wa vyombo vyote vya habari. Katika mwaka uliopita, tulikamilisha mtandao wetu wa kukusanya habari duniani, ili kuongeza uwezo wetu wa kuripoti habari zinazofuatiliwa. Pia tumeongeza lugha zetu za kutangaza kutoka 44 hadi 68, na kuzihudumia nchi na sehemu 233 duniani. Katika ripoti kuhusu mgogoro kati ya Russia na Ukraine, janga la UVIKO-19, tulitangaza kwa uwazi na kufuata ukweli, na kueneza misimamo na mipango sahihi na ya haki ya China kwa jumuiya ya kimataifa.

Katika mwaka mpya, tutaendelea na juhudi zetu kwa ujasiri, na kuonesha hali mpya ya China katika zama mpya katika pande zote kwa jumuiya ya kimataifa. Huu pia ni mwaka wa 10 tangu China itoe pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”. Tutaendelea kujipatia marafiki wa vyombo vya habari, kuhimiza mawasiliano ya staarabu, ili kubeba majukumu ya kuenzi thamani ya pamoja ya binadamu na kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.

Nawatakieni heri ya mwaka mpya, maisha bora na usalama, Asanteni!