Xi Jinping atuma salama za pongezi kwa rais mpya wa Uswisi Alain Berset
2023-01-01 19:09:54| CRI

Rais Xi Jinping wa China ametuma salama za pongezi kwa rais mpya wa Uswisi Alain Berset.

Rais Xi amesema, chini ya moyo wa “usawa, uvumbuzi na kunufaishana”, uhusiano kati ya China na Uswisi umedumisha mwelekeo mzuri wa maendeleo, uaminifu wa kisiasa kati ya pande mbili unaimarishwa siku hadi siku, na ushirikiano wa kiutendaji kwenye sekta mbalimbali unaendelea kuhimizwa. Amesema anatilia maanani sana maendeleo ya uhusiano kati ya China na Uswisi, na kupenda kushirikiana na rais Berset katika kuhimiza kupata maendeleo mapya juu ya uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa kiuvumbuzi kati ya pande hizo mbili, na kunufaisha nchi mbili pamoja na wananchi wake.

Wakati huohuo, makamu wa rais wa China Wang Qishan amempongeza Viola Amherd kwa kuchaguliwa kuwa makamu wa rais wa Uswisi.